Ben Paul anakuja kivingine

Monday December 31 2018

 

By OLIPA ASSA

MSANII wa muziki wa R$B, Ben Paul amesema anaingia 2019 kwa kishindo cha kazi zitakazoandika rekodi ya aina yake, akitaja vitu vya kuzingatia kwenye nyimbo zake kuwa ni ujumbe utakaogusa watu wa rika zote.
Ben Paul anasema anaamini aina ya muziki anaoimba hakuna wa kushindana naye, hivyo 2019 utakuwa mwaka wa kuongeza rekodi ya aina yake kwa mashabiki wa muziki nchini.
"Mwaka 2018 nimeutendea haki kwa kuachia nyimbo mbalimbali ambazo zimepokelewa na mashabiki kama 'Sio Mbaya, 'Ntala Nawe na nyinginezo ambazo nimewashirkisha wasanii wa filamu kama  Jacqueline Wolper na Yvonne Cherly 'Monalisa.
"Najipanga kuhakikisha nakuja kivingine zaidi kwani sitaki kuzoeleka kuonekana ni Ben Paul yule yule kila mwaka, naamini nitafanya kitu cha kuwa mfano kwa watu wengine,"anasema.Advertisement