Singida United waliamsha tena kwa Yanga

Muktasari:

Ushindi wa leo Jumatano dhidi ya Yanga, utaonyesha sura mpya ya kuimarika kwao kwani utakuwa wa pili mfululizo.

Dar es Salaam. Singida United inayoundwa na wachezaji wakongwe leo Jumatano itacheza dhidi ya Yanga wakiwa na matumaini ya kuendeleza wimbi lao la ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Liti, Singida.

Singida United baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wakongwe Athumani Idd 'Chuji', Haruna Moshi 'Boban', Ame Ali walioungana na Haji Mwinyi Ngwali, Six Mwasekaga, Tumba Lui na Muharami Issa 'Marcelo' imebadilika.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha, Ramadhani Mswazurwino kinapambana kujiondoa mkiani mwa ligi na ujio wa nyota hao umeanza kutoa tumaini jipya kwao baada ya kuichapa kuichapa Ruvu Shooting 1-0.

Akizungumzia hilo mshambuliaji, Mwasekaga alisema ni ushirikiano na wameamua kufanya kazi: "Kila kitu ni uamuzi na kujituma."

Ushindi wa leo Jumatano dhidi ya Yanga, utaonyesha sura mpya ya kuimarika kwao kwani utakuwa wa pili mfululizo.

Singida United inashika nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na pointi 10, baada ya kucheza mechi 16,   Ndanda FC inashika mkia na pointi tisa imecheza mechi 17.

Inacheza na Yanga iliyo nafasi ya nane na pointi 25, baada ya kucheza mechi 14. Simba ndio vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamecheza mechi 16 na kujikusanyia pointi 41.

Yanga yenyewe inakutana na Singida United baada ya kupoteza mechi mbili mfulurizo kutoka kwa Kagera Sugar walipigwa 3-0 na wakacjhapwa na Azam FC 1-0.