Real yafanya kufuru Copa del Rey

Friday December 7 2018

 

Madrid, Hispania. Baada ya kung’olewa mapema katika mashindano ya Copa del Rey msimu uliopita Real Madrid msimu huu imefanya kufuru.

Kikosi hicho cha Kocha Santiago Solari jana Alhamisi kiliibamiza timu ya Daraja la Tatu ya Melilla kwa mabao 6-1 hivyo kusonga kwa jumla ya mabao 10-1.

Ushindi huo wa jumla umeiingiza Real katika hatua ya 16, bora ya mashindano hayo ya pili kwa mvuto baada ya La Liga.

Mabao yaliyoipa ushindi huo jana yalifungwa na Marco Asensio na Isco kila mmoja mawili, Javi Sanche na Vinicius Junior wakati lile la kufutia machozi la wageni lilifungwa na Melilla kwa penalti baada ya Yacine Qasmi kuangushwa ndani ya penalti.

Pamoja na kocha Solari kufanya mabadiliko ya wachezaji kumi kati ya nyota wake wa kikosi cha kwanza walioichapa Valencia 2-0 Jumamosi iliyopita bado matokeo yalikuwa mazuri.

Timu hiyo kwa sasa inasubiri mechi za awali zimalizike ili ratiba ya 16, bora ipange ajue atakutana na timu ipi lakini kuna kila dalili akaziepuka Atletico Madrid na Barcelona katika hatua inayofuata.  

 

 

Advertisement