Yanga yaendelea kujifua Njombe

Tuesday September 12 2017

By GIFT MACHA

Njombe. Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua kwenye Uwanja wa Chai Chai mjini hapa kabla ya kuikabili Majimaji mwishoni mwa wiki.
Jana Jumatatu jioni kocha wa Yanga, George Lwandamina aliwapa mazoezi mepesi nyota walioanza dhidi ya Njombe, huku wale waliokuwa benchi wakifanya mazoezi makali.
Kocha huyo raia wa Zambia alisema kuna vitu vichache lazima wavifanyie kazi kabla ya kukabiliana na Majimaji ambayo ilitoka sare na Prisons wikiendi iliyopita.
"Siwezi kusema wazi ni marekebisho gani lakini lazima tuongeze nguvu kwenye vitu vya kiufundi," alisema Lwandamina.