Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

West Ham yamfuta kazi bosi wa usajili fasta

Bosi Pict

Muktasari:

  • West Ham United, ambayo usiku huo wa Jumatatu ilikuwa na mechi ya Ligi Kuu England na kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Chelsea, ilibainisha kwamba bosi huyo Mjerumani anaondoka kwenye timu yao baada ya kocha mpya, Graham Potter kuja na mtaalamu wake wa masuala ya usajili, Kyle Macaulay.

LONDON, ENGLAND: WEST Ham United imethibitisha kumfuta kazi bosi anayehusika na usajili, Tim Steidten ndani ya saa 12 tangu dirisha dogo la uhamisho wa wachezaji kufungwa usiku wa juzi Jumatatu.

West Ham United, ambayo usiku huo wa Jumatatu ilikuwa na mechi ya Ligi Kuu England na kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Chelsea, ilibainisha kwamba bosi huyo Mjerumani anaondoka kwenye timu yao baada ya kocha mpya, Graham Potter kuja na mtaalamu wake wa masuala ya usajili, Kyle Macaulay.

Mwenyekiti wa klabu hiyo ya London, David Sullivan alihusika kwa kiasi kikubwa katika usajili wa dirisha dogo na walifanikiwa kunasa huduma ya straika, Evan Ferguson kwa mkopo kutoka Brighton, dili hilo likikamilika dakika za mwisho kabisa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

"Klabu ya soka ya West Ham United inathibitisha kwamba mkurugenzi wa ufundi Tim Steidten ataondoka kwenye timu. Tim alikuwa mtu muhimu kwenye idara yetu ya usajili. Ujio wa kocha wetu mpya, Graham Potter, amekuwa na mkuu mwingine wa kitengo cha usajili, hivyo tumemruhusu Tim akatafute fursa kwingineko. Tunapenda kumshukuru Tim kwa kazi yake na tunamtakia kila la heri."

Steidten alijiunga na klabu hiyo ya London mwaka 2023 baada ya kupata mafanikio makubwa Bayer Leverkusen na Werder Bremen. West Ham imetumia karibu Pauni 250 milioni kusajili wachezaji wapya katika kipindi cha uongozi wa bosi huyo Mjerumani.