Wanyama: Mkenya wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya Uingereza

By Maliki Muunguja, Mwanaspoti
Kenya kwa ujumla imekuwa ikipitia wakati mgumu kuzalisha nyota wa mpira wa miguu wenye hadhi ya kimataifa, lakini wakati Victor Wanyama alipokuwa Tottenham Hotspur, alikuwa ni nyota halisi wa ulimwengu.
Nyota ya Wanyama tangu ahamie katika Ligi ya Soka nchini Marekani (MLS) imeonekana kufifia, tofauti na moto aliouwasha wakati akiwa na Spurs katika Ligi Kuu ya Soka Uingereza.
Maisha ya soka ya Wanyama pale Spurs yalikuwa mafupi na yaliyoandamwa na majeraha mengi, lakini alipokuwa mzima wa afya na kupata fursa ya kucheza, alionekana kuwa mhimili mkubwa katika dimba la kati kama kiungo.
Akicheza pacha na Mbelgiji mnyumbulifu Moussa Dembele, Wanyama alikuwa sehemu ya wachezaji wawili tishio wa kiungo cha kati, akitengeneza mazingira mepesi kwa washambuliaji kwa wafumania nyavu kama vile Christian Erikssen kucheza kwa uhuru katika dimba la juu.
Wakati wake bora akiwa na jezi ya Tottenham, ulikuwa ni ule ambao alipiga shuti la umbali mrefu dhidi ya Liverpool huko White Hart Lane, lakini pia aliweza kuonyesha kiwango kikubwa zaidi akiwa na uzi wa timu hiyo yenye makazi yake London Kaskazini.
Mkenya huyo mwenye futi 6 na inchi 2 alikuwa mkakamavu na mwenye nguvu katika kukaba, lakini pia alikuwa na akili nyingi katika kuchezea mpira, na alikuwa mhimili wa kutumainiwa katika mfumo wa kocha Maurichio Pochettion wa kucheza kwa kukabia juu na upigaji pasi za haraka wakati wa misimu yake ya kwanza klabuni hapo.
Pochettino alishamfundisha Wanyama akiwa Southampton, na wawili hao waliungana tena huko London Kaskazini wakati Spurs walipolipa Pauni milioni 11 kwa mchezaji huyo katika msimu wa joto wa mwaka 2016.
Wanyama alikuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Tottenham, na akianza katika michezo 35 ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza na kuisaidia kilabu kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya kuuanza msimu kwa michezo kadhaa ambayo ilionyesha matumaini makubwa kwa watu, nyota ya Wanyama ikaanza kufifia katika misimu kadhaa mfululizo kutokana na majeraha.
Katika misimu mitatu iliyofuata, Nyota huyo wa  Harambee Star alicheza mechi 33 tu ya ligi kwa Tottenham kabla ya kuondoka kutimkia zake Marekani Machi 2020.
Kwa jumla, Mkenya huyo alicheza michezo 97 kwa Spurs katika mashindano yote, akiingia wavuni mara saba. Alikuwa sehemu ya kikosi kilichopata medali ya nafasi ya pili ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2019.
Mbali na michango yake uwanjani, Wanyama fursa mpya ya mashabiki wa Spurs. Akiwa Southampton, alikuwa Mkenya wa kwanza kucheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, na kuwavutia mashabiki wengi kushabikia klabu hiyo ya St. Mary.
Haishangazi, Wakenya wenzake kuhama naye hadi London Kaskazini wakati yeye akihamia Spurs mwaka 2016.
Spurs haikuweza kurudisha fadhila na ilishinda mechi nyingi, lakini kwa bahati mbaya, klabu hiyo haikutwaa taji lolote wakati Wanyama akiichezea.
Hayo yanabaki kuwa moja ya majuto makubwa kwa mchezaji huyo.

"Inasikitisha," Wanyama aliiambia MLSsoccer.com. "Nilijuta kuondoka vile, naomba radhi kwa mashabiki na mimi mwenyewe baada ya kuwa na timu bora, tukicheza katika kiwango bora, lakini tukashindwa kupata taji lolote. Ni aibu tu, inauma kuondoka bila chochote. "
Katika misimu yake mitatu kamili huko Spurs, Tottenham ilimaliza nafasi ya pili, wa tatu na wa nne kwenye Ligi Kuu, huku wakipoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool mwaka 2019.
Hizo zilikuwa siku ambazo Spurs walikuwa wanakaribia kupata walau taji lolote, na mashabiki wa mpira wa Kenya waliamini kweli kwamba hivi karibuni wangeweza kumsherehekea bingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kutoka nchini kwao.

Wakenya wengi walikuwa wakiwaunga mkono Wanyama na Spurs kwenye tovuti za kubashiri nchini Kenya. Hilo ndilo lililokuwa tumaini na imani yao kwenye timu.

Pengine Wanyama asingekuwa na bahati mbaya ya majeraha, Spurs wangeweza kushinda taji zaidi ya moja katika mashindano yote yale.

Kwa kutazama nyuma msimu huo wa kwanza, msimu wa mwisho wa Spurs huko White Hart Lane, na ubora thabiti aliouonyesha, mashabiki wa Tottenham wanaweza kusamehewa kwa kuhisi mabadiliko mafupi ya mambo ambapo hawakuweza kuona ubora zaidi kutoka kwa Mkenya huyo katika ukamilifu wake.