Van Dijk apata hofu Liverpool
Muktasari:
- Van Dijk alisema hawezi kukimiliki kichwa cha kila mchezaji kwa maana ya kumtaka kuwa mtulivu kutokana na kelele zinazopigwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wapo kwenye nafasi kubwa ya kikosi chao chini ya kocha Arne Slot kwenda kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa kati na nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk amesema ameanza kupata wasiwasi kutokana na wachezaji wenzake kuvurugwa na kelele nyingi zinazopigwa dhidi yao juu ya uwezekano wa kunyakua ubingwa msimu huu.
Van Dijk alisema hawezi kukimiliki kichwa cha kila mchezaji kwa maana ya kumtaka kuwa mtulivu kutokana na kelele zinazopigwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wapo kwenye nafasi kubwa ya kikosi chao chini ya kocha Arne Slot kwenda kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Kichapo kutoka kwa Tottenham Hotpur kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi Jumatano iliyopita kilikuja baada ya sapraizi kubwa katika sare dhidi ya Manchester United kwenye Ligi Kuu England, Jumapili iliyopita.
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Liverpool kucheza mechi mbili bila ya ushindi tangu iwe chini ya kocha Slot na beki wa kati Van Dijk ameanza kuwa na wasiwasi, lakini akiamini hilo halitakuwa shida kwao na kuwandoa kwenye mipango ya kufukuzia mataji manne msimu huu.
“Msisikilize kelele zinazopigwa huko nje kwa sababu msimu ndio kwanza unaanza,” alisema Van Dijk akituma ujumbe huo kwa wenzake.
Alipoulizwa kama baadhi ya wachezaji Liver wanakabiliana na presha, Van Dijk alisema: “Ni wazi, hakika. Mitandao ya kijamii ni tatizo kubwa na ni sehemu ya maisha ya watu kwa sasa. Siwezi kumzuia kila mchezaji kuwa na hisia zake.