UEFA kuanzisha mashindano ya wakimbizi

UEFA kuanzisha mashindano ya wakimbizi

SHIRIKISHO la Soka Barani Ulaya (UEFA) limetangaza kuanza kwa mashindano ya Kimataifa ya Soka kwa wakimbizi 'Unity Euro Cup' mwishoni mwa mwezi huu likishirikiana na Shirikila la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR.

Mashindano hayo yatahusisha timu 8 huku asilimia 70 ya timu hizo zitakuwa na wachezaji ambao ni wakimbizi na asilimia 30 ya wasio wakimbizi.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika mji wa Nyon nchini Uswisi ambako ndiko yalipo makao makuu ya UEFA.

Timu zitakazoshiriki michuano hiyo ya kirafiki zinatoka nchi za Austria, Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Malta, Ireland na Switzerland.

Tangazo hilo lilitolewa rasmi jana Juni 20 ikiwa ni siku ya wakimbizi Duniani huku lengo kubwa ni kuimarisha uhusiano kati ya wakimbizi na jamii walizohamia kwa kupitia nguvu ya soka.