Telles atua Sevilla kwa mkopo

Wednesday August 03 2022
telles pic

MANCHESTER, ENGLAND.  BEKI wa Manchester United, Alex Telles amejiunga na Sevilla kwa mkopo wa msimu mzima hadi mwaka 2023.
Aidha kwenye mkataba huo hakuna kipengele cha beki huyo kununuliwa jumla na Sevilla, baada ya makubaliano pande zote.
Telles atasaini mkataba wa kukipiga wa Sevilla mapema wiki hii kabla ya kutambuliswa rasmi.
Mbrazil huyo alikubali kujiunga na Sevilla kwa mkopo, kutokana na ukweli kwamba beki huyo atakosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag msimu huu.
Ujo wa Tyrell Malacia umetibua uwezekano wa beki huyo kupangwa kikosi cha kwanza msimu huu, kwani ni chaguo namba moja wa Ten Hag.

Advertisement