Samatta moto umewaka

Mshambuliaji wa Fenerbahce, Mbwana Samatta ameuanzisha moto wake wa kutupia baada ya jana kufunga bao moja kati ya matatu yaliyowahakikishia alama tatu muhimu.

Samatta amekaa nje kwa zaidi ya wiki tano akisumbuliwa na majeraha ya misuli ya pembeni ya goti  amerejea uwanjani na kufunga katika mechi mbili mfululizo alizocheza.

Alianza mechi ya kwanza dhidi ya Kasimpasa na jana akaweka tena dhidi ya Ankaragucu kwa bao la ufundi na wamesalia nafasi ya pili wakiwa na alama 38 wakiwa nyuma ya Bestikas wenye alama 38 wakitofautiana mabao manne.

Samatta ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars huenda kaanza kukipiga na staa maarufu duniani, Mesut Ozil katika klabu hiyo baada ya kukamilisha usajili wake akitokea Arsenal.