Perez afunguka kuhusu Super League

MADRID, HISPANIA. RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema European Super League ina lengo zuri juu ya maendeleo ya mpira wa miguu na wanatarajia itaanza kutimua vumbi Agosti mwaka huu.
Perez, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa michuano hiyo amekuwa kiongozi wa kwanza kati ya zile timu 12 zilizo thibitisha kushiriki yeye akijitokeza hadharani na kuongelea ishu hiyo katika mahojiano aliyofanya na moja ya televisheni huko Hispania.
"Mpira unatakiwa uwe kama kampuni, maisha yamebadilika na watu pia wamebadilika tunatakiwa kuendana na wakati tuliopo
"Mashabiki wanaonekana kupoteza mvuto na mpira wa miguu. Kuna mechi nyingi ambazo hazina ubora jambo linalosababisha watoto wadogo wanaochipukia kutokuwa na mapenzi juu ya mpira,
"Ikiwa mashabiki wanapungua, hata thamani ya soka nayo inapungua hivyo tumeona kuna haja yakufanya jambo kama hili, vilevile baada ya  janga la Corona ambalo limechangia hasara ya zaidi Bilioni 4.3 milioni  kwa timu huku Madrid tukipata hasara ya Pauni 350 milioni, kila kitu kilikuwa kimebadilika,"alisema Perez na kuongeza,
"Lakini mpira wa miguu unapendwa Duniani kote. timu 12 ambazo zimekubali kuingia kwenye michuano hii zina mashabiki Ulimwenguni kote, tumeanzisha kitu  tutakachowapeleka mezani na kuwafanya wapende tena kuangalia soka."alimaliza.