Pep anabaki Man City

Friday November 20 2020
pep pic

MANCHESTER, ENGLAND. HIZI ni habari mbaya kwa mashabiki na mabosi wa Barcelona. Ndio, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekubali kusaini mkataba mpya kuendelea kuwanoa wababe hao wa Etihad.

Awali, kulikuwa na sintofahamu kuhusu hatima ya Pep, ambaye alikuwa amebakiza miezi saba tu katika mkataba wake wa sasa huku wakala wake akisuasua kuanza mazungumzo ya dili jipya. Lakini, jana alithibitisha kuwa atasaini mkataba mpya na mrefu na hilo, linaongeza kasi ya supastaa wa Barcelona, Lionel Messi kuwa njiani kwenda kuungana naye pale Etihad.

Tayari Messi ameeleza kuchoshwa na maisha ndani ya Barcelona hasa kubebeshwa lawama kila wakati mambo yanapoharibika.

Messi ataondoka bure mwishoni mwa msimu huu kulingana na kipingele cha mkabata.


Advertisement