Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Papiss Cisse amtosa Miss Newcastle

NEWCASTLE, ENGLAND

STAA wa Newcastle United na timu ya taifa ya Senegal, Papiss Demba Cisse, inasemekana amemtosa mpenzi wake, Rachelle Graham ambaye ni Miss Newcastle wa zamani kwa kile alichokiita ‘kutaka kujikita zaidi katika soka’.

Wawili hao walikuwa katika penzi maarufu zaidi katika Jiji la Newcastle, lakini inasemekana Cisse amemtosa mrembo huyo huku akimwacha katika wakati mgumu kutokana na mrembo huyo kujiandaa kuishi pamoja na Cisse.

Achilia mbali penzi lao, wawili hao walikuwa bega kwa bega katika shughuli za kijamii,  mapema mwaka huu, wote wawili walishirikiana katika kusaka gari la wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya kupeleka katika kijiji alichozaliwa Cisse nchini Senegal.

Kwa sasa, Rachelle yuko katika hali mbaya akiwa amevunjwa moyo na kitendo cha Cisse kumtosa huku akidai kujikita zaidi katika soka baada ya kile alichosema kukosa kufanya mazoezi ya kutosha wakati wa maandalizi ya msimu mpya.

Cisse aligoma kutinga katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo baada ya kukataa jezi za wadhamini wapya wa timu hiyo kwa madai kwamba imani yake ya kidini ilikuwa haimruhusu kutangaza kampuni zinazotoza riba.

Hata hivyo, baadaye nyota huyo aliibukia katika Casino moja jijini humo hali iliyozua shaka kuhusu imani yake ya dini yake ya Kiislamu ambayo pia inakataza uchezaji kamari.

Inadaiwa Rachelle yuko hoi na amekuwa akifanya jitihada za kurudiana na nyota huyo wa Senegal ambaye analipwa kiasi cha Pauni 40,000 kwa wiki na Newcastle.

“Rachelle amevunjika moyo sana na anajaribu kila awezalo kurudiana na Papiss. Hakutaka uhusiano huu uvunjike,” alisema mmoja wa rafiki zake.

Wakala wa mchezaji huyo hakutaka kusema lolote kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo huku akisema suala hilo ni habari binafsi kati ya Cisse na Rachelle.

Mrembo huyo naye alikataa kusema lolote kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na Cisse akisema: “Si suala la mtu mwingine. Napenda kutosema lolote kuhusu jambo hilo.”