Moyes arejea Everton na rekodi

Muktasari:
- Rekodi hiyo ni ya kuwa kocha wa 11 kurejea katika klabu aliyoiwahi kuinoa katika ligi tano kubwa Ulaya.
LIVERPOOL, ENGLAND: Everton juzi imetangaza rasmi kumrejesha David Moyes kuwa meneja wake huku kocha huyo akiingia katika historia kutokana na urejeo huo.
Rekodi hiyo ni ya kuwa kocha wa 11 kurejea katika klabu aliyoiwahi kuinoa katika ligi tano kubwa Ulaya.
Moyes aliinoa Everton mara ya kwanza kuanzia 2002 hadi 2013 kisha kutimkia Manchester United na sasa amerejea katika timu hiyo akichukua mikoba ya Sean Dyche aliyetimuliwa.
Makocha wengine waliowahi kufanya hivyo ni Jose Mourinho ambaye aliifundisha Chelsea kuanzia 2004 hadi 2007 na kisha akaifundisha tena kuanzia 2013 hadi 2015 na kuna Roy Hodgson aliyeinoa Crystal Palace kwa awamu mbili tofauti.
Harry Redknapp amewahi kuinoa Portsmouth katika awamu mbili tofauti kama ilivyowahi kutokea kwa Tony Pulis na Stoke City.
Makocha wengine na timu ambazo wamewahi kuzinoa timu kwa awamu tofauti ni Kevin Keegan (Newcastle United), Kenny Dalglish (Liverpool), Carlo Ancelotti (Real Madrid), Zinedie Zidane (Real Madrid), Claudio Ranieri (AS Roma) na maximilliano Allegri (Juventus)