Mount apiga tatu, Chelsea ikiipiga wiki Norwich

Saturday October 23 2021
chelsea pic

KIUNGO wa Kiingereza, Mason Mount amepachika mabao matatu wakati klabu yake ya Chelsea ikiishushia mvua ya mabao 7-0 Norwich kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao umechezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Norwich ambao walionekana kuzidiwa kwenye mchezo huo tangu kipindi cha kwanza, waliruhusu nyavu zao kutikiswa dakika ya nane na Mount aliyepokea pasi safi ya mwisho kutoka kwa Jorginho.

Licha ya kuwa mbele kwa bao hilo la mapema, Chelsea ambayo imcheza mchezo huo bila ya kuwa na washambuliaji wao muhimu, Timo Werner na Romelu Lukaku kutokana na kusumbuliwa na majeraha, waliendelea kulisakama lango la Norwich ambao wanaburuza mkia kwenye msimamo wa EPL.

Dakika 10 baadae Chelsea ipata bao la pili kupitia kwa Hudson-Odoi  aliyetokea winga ya kushoto kufuatia kupenyezewa pasi na Mateo Kovacic.

Kabla ya kwenda mapumziko Chelsea ilipata bao la tatu lililofungwa na beki wake, Reece James huku asisti ya bao hilo ikitolewa na Mount.

Jahazi la Norwich liliendelea kuzama kipindi cha pili kwani walijikuta wakiruhusu mabao manne ikiwemo moja ambalo walijifunga wenyewe dakika ya 62 kupitia kwa Aarons M. mabao mengine ya matajiri hao wa London yalifungwa na Chilwel na Mount aliyetupia mawili dakika ya 85 na 90+1.

Advertisement


Chelsea: Mendy, Chalobah, Thiago Silva, Rudiger, James, Jorginho, Kovacic, Chilwell, Hudson-Odoi, Mount, Havertz.

Subs: Arrizabalaga, Alonso, Christensen, Loftus-Cheek, Saul, Barkley, Ziyech, Azpilicueta, Sarr.

Kocha: Thomas Tuchel

Goals: Mount (8, 85, 91), Hudson-Odoi (18), James (42), Chilwell (57), (Aarons 62og).  

 
Norwich: Krul, Kabak, Gibson, Hanley, Aarons, Lees-Melou, Normann, McLean, Giannoulis, Sargent, Pukki.

Subs: Rupp, Dowell, Rashica, Tzolis, Sorensen, Williams, Gunn, Idah, Omobamidele.

Kocha: Daniel Farke

Red-cards: Gibson (65)

Advertisement