Morocco yamtimua Enrique Hispania

MADRID, HISPANIA. Kocha Luis Enrique amejiuzulu nafasi ya ukocha mkuu wa taifa la Hispania baada ya kuondoshwa kwenye Faina za Kombe la Dunia 2022 hatua ya 16 bora na Morocco.
Enrique (52) alichukua mikoba ya kuinoa Hispania 2018 na kufanikiwa kuifikisha nusu fainali ya Euro 2020.
Kocha huyo ameshindwa kuipeleka Hispania hatua ya robo fainaili, baada ya kuondolewa raundi ya 16 bora ilipocheza dhidi ya Morocco.
Hispania iliondolewa kwa mikwaju wa penalti 3-0 kipa wa Morocco, Yassine Bounou akiibuka kinara baada ya kupangua penalti mbili kwenye mchezo huo.
Kwa mujibu wa ripoti Enrique anajiandaa kurejea katika soka la ngazi ya klabu baada ya kuitema Hispania.
Wakati huo huo Hispania imemteua Luis De la Fuente kuwa kocha mkuu akichukua nafasi ya Enrique taarifa imeripotiwa. Makubaliano kati ya Shirikisho la Hipania na kocha huyo yamekamilika baada ya kusaini mkataba. 
De la Fuente alikuwa akiinoa timu ya vijana ya Hispania chini ya umri wa miaka 21 kabla ya kupewa majukumu ya kukinoa kikosi cha wakubwa.