Mechi zilizompa rekodi Ronaldo

BUDAPEST, HUNGARY. KAMA ulidhani mshumbuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo amekwisha basi unajidanganya kwani jamaa ilimchukua dakika 3, tu kuvunja rekodi ya michuano ya Ulaya (EURO) iliyodumu kwa takribani miaka 37.

Iko hivi, Ronaldo aliweka rekodi hiyo baada ya kutupia mabao mawili na kuisaidia timu yake ya Ureno kuanza vyema harakati za kulitetea taji hilo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Hungary.

Katika mchezo huo uliokuwa mgumu uliwachukua Ureno kusubri dakika sita  za mwisho wa mchezo kwa kuanza kujiandikia bao la kwanza dakika ya 84, kupitia kwa Raphael Guerreiro kisha Cristiano Ronaldo kupachika bao la pili dakika ya 87 kwa njia ya penalti  kabla ya kufunga bao la tatu dakika ya 90.

Ronaldo ameandika historia ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Euro, rekodi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Mfaransa Michael Platini aliyekuwa akiongoza kwa kuwa na mabao 9, kwenye (EURO) ya 1984.

Ilimchukua Ronaldo misimu 5, tofauti kuvunja rekodi hiyo, huku akileta matumaini kwa timu yake ya taifa ya kulitetea tena taji hilo baada ya kulichukua mwaka 2016, Nchini Ufaransa. Mwanaspoti inakuletea  magoli yote ya Ronaldo kwenye michuano ya Euro.

1.  vs UGIRIKI, (EURO 2004) HATUA YA MAKUNDI
Hili lilikuwa ni goli lake la kwanza kwenye michuano hii kwa kuwashangaza wenyeji Ugiriki.

2. vs UHOLANZI, (EURO 2004) HATUA YA NUSU FAINALI
Alimtungua golikipa wa zamani wa Manchester United Edwin Van Der Sar, kisha akaihakikishia Ureno  kutinga fainali ingawa walichezea kichapo kutoka kwa wenyeji Ugiriki.

3. vs JAMHURI YA CZECH, ( EURO 2008) HATUA YA MAKUNDI
Hakuwa na bahati sana kwenye michuano hii kwani alifunga bao moja tu dhidi ya Jamhuri ya  Czech.

4. vs UHOLANZI (EURO 2012) HATUA YA MAKUNDI
Alifunga bao moja dhidi ya Uholanzi na kufunga bao lingine dhidi ya Ukraine.

5. vs UHOLANZI (EURO 2012) HATUA YA MAKUNDI
Akiwa na Klabu ya Real Madrid wakati huo aliisaidia timu yake ya taifa kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwa kuitoa Uholanzi.

6. vs JAMHURI YA CZECH (EURO 2012) HATUA YA ROBO FAINALI

Goli lake la kuzamia kama yupo majini dhidi ya jamhuri ya Czech liliisaidia timu yake kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

7. vs HUNGARY (EURO 2016) HATUA YA MAKUNDI
Ureno ilipata tabu sana katika mchezo huu lakini  Cristiano Ronaldo alifanikiwa kufunga bao.

8. vs HUNGARY ( EURO 2016) HATUA YA MAKUNDI
Alipiga kichwa cha maana na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya 16 bora.

9. vs WALES ( EURO 2016) HATUA YA NUSU FAINALI
Alifunga gili bora la kichwa dhidi ya Wales na kuisaidia timu yake kutinga fainali na kufanikiwa kuchukua taji hilo baada ya kuwachapa Ufaransa waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo.

10. vs HUNGARY ( EURO 2020) HATUA YA MAKUNDI

Hapa ndipo alipoandika rekodi yake kwa ya kufikisha magoli 10, kwenye michuano hii, pia akaikisha magoli 106, kwa ngazi ya timu ya taifa huku akiwa amebakisha magoli 4 tu kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa Iran Ali Daei mwenye magoli 109.