Man United hatihati kujitoa kwenye dili la Ramos

MADRID, HISPANIA. MABOSI wa Manchester United  wameripotiwa kuwa huenda wakajitoa kwenye harakati za kuiwania saini ya beki kisiki wa Real madrid Sergio Ramos aliyeachana na wababe katika dirisha hili.

taarifa ya kuondoka kwa beki huyo mwenye miaka 35 ilifahamika jumatano jioni huku nyota huyo akishinda mataji 22 katika miaka 16 aliyohudumu na mabingwa hao wa Hispania.

Licha ya Man United,PSG na Manchester City ni miongoni mwa klabu zilizo kwenye orodha ya kuitaka saini ya beki huyo anayeondoka Real madrid kama mchezaji huru akiwa amecheza michezo 671 katika miaka 16 tangu ajiunge mwaka 2005 akitokea Sevilla.

Sababu za Man united kusitisha mpango wa kumsajili inasababishwa na bifu lililokuwepo kati ya kaka yake Ramos, Rene Ramos  ambaye hana uhusiano  mzuri na Mtendaji mkuu wa timu hiyo Ed Woodward na sababu kubwa imetokana na  kitendo cha Rene kukwamisha dili la Ramos kutua Man United mwaka 2016.

Man United imekuwa na mapungufu makubwa kwenye eneo lake la ulinzi hali inayosababisha kocha wao Ole Gunnar Solskjer kuhitaji kusajili beki wa kati katika dirisha hili na Ramos alionekana kuwa mmoja ya wachezaji ambao huenda wangesajiliwa.

Ramos ambaye alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Madrid kwenye kipindi cha hivi karibuni anaondoka kwenye timu hiyo kwa kile kinachoeleza kwamba hakukuwa na maelewano kati yake na rais wa timu hiyo Florentino Perez.