Mama Ronaldo alia mwanae akifunga mbili

Sunday September 12 2021
mama pic

MANCHESTER, ENGLAND. MAMA yake mzazi Cristiano Ronaldo, Maria Dolores dos Santos Aveiro amelia machozi ya furaha baada ya mtoto wake kipenzi, kufunga mabao mawili kwenye uwanja wa Old Trafford.

Tukio hilo limetokea kwenye mechi ya Ligi ya Kuu England, Man United ilipomenyana na Newcastle United ilipoichapa mabao 4-1.

Ronaldo, 36, aliwakonga nyoyo mashabiki wa Manchester United waliofurika uwanjani kumshudia baada ya kurejea Old Trafford akitokea Juvetus.

mama pic 1

Kamera zilizopo uwanjani zilimuonyesha mama huyo akifuta machozi baada ya kushindwa kujizuia furaha yake.

Ronaldo alicheza mechi yake ya kwanza Old Trafford tangu alipoondoka miaka 12 iliopita alipojiunga na Real Madrid.

Advertisement


Advertisement