Madrid yaweka rekodi tamu

MADRID, HISPANIA. REAL Madrid imeweka rekodi ya kubeba makombe matano ya UEFA Super Cup, usiku wa kuamkia leo baada ya kuifunga Eintracht Frankfurt mabao 2-0.
Mechi hiyo iliyopigwa katika jiji la Helsinki, Finland imezikutanisha bingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya na Europa wa msimu uliyopita.
David Alaba alifungua kalamu ya mabao kwa upande wa Real Madrid, kabla ya Karim Benzema kupachika bao la pili dakika ya 65.
Mkali huyo wa mabao Los Blancos alifikisha jumla ya mabao 324 akimpiku mkongwe Raul, kwenye orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo akiwa kinara kwani aliweka wavuni jumla ya mabao 450 kipindi anakipiga.
Sasa Real Madrid itakua na kibarua cha kwanza La Liga wekiend hii, katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Almeria.