Ligue 1 yeyote anashuka
PARIS, UFARANSA. MAMBO ni mengi Lique 1 ya Ufaransa. Kwenye msimamo wa Ligi Kuu eneo la juu ni kama kimeshaeleweka. PSG kashikilia vyema usukani na suala la kuwa bingwa ni mechi kadhaa tu zinahesabiwa. Hakuna ubishi, haina mpinzani.
Hata hivyo, bado kuna ligi nyingine haijaisha nayo ni ile ya timu zinazoshika nafasi za chini. Kuanzia timu iliyopo nafasi ya 13 hadi ya mwisho kwenye msiamo hakuna yenye uhakika wa kumaliza salama. Hakieleweki. Yeyote anabaki, yeyote anashuka.
Clermont inayoshika nafasi ya mwisho inaweza kupanda hadi nafasi ya 14 ikiwa itashinda mechi mbili za mwanzo na timu zinazoifuatia za juu yake zikafungwa au kutoa sare.
Utamu wa vita hiyo ni Le Havre inayoshika nafasi ya 13 itacheza na Montpellier iliyopo nafasi ya 14, utofauti wa alama baina yao ni moja tu, hivyo kama Montpellier ikishinda inaweza kusogea hadi nafasi ya 13 au 12 ambayo inashikiliwa na Strasborug.
Metz ambayo ipo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja ikiwa na alama zake 23 inaweza kupanda hadi nafasi ya 14 ikiwa itashinda mechi dhidi ya Monaco na timu nyingine zilizopo juu yake zikafungwa au kutoka sare.
Nantes ambayo ipo eneo la kucheza mtoano ikishinda dhidi ya Nice itafikisha pointi 28 na kuishusha Strasborug au Le Havre ikiwa mojawapo itamfungwa mwenzake.