Leicester yaiwekea ngumu Chelsea

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Leicester City, Brendan Rodgers amekiri kwamba Wesley Fofana, hatauzwa kwa bei chee na thamani yake ni Pauni 80 milioni.
Rodgers ameionya Chelsea na kwani iliipiga chini ofa  yao ya Pauni 65 milioni iliyotolewa tangu wiki iliyopita.
Rodgers alisema; “Nilikua sifahamu kama ofa mbili zilitumwa, jambo la kusisitiza, Fofana hatauzwa kwa bei rahisi, hilo ni jambo la msingi kwetu kwa sasa,”
Rodgers amepigilia msumari kwamba Fofana ni mchezaji bora wa Leicester na anataka abaki zaidi ya msimu mmoja.
Fofana ameendelea na mazoezi kama kawaida akiwa na klabu yake ya sasa lakini haijulikani Chelsea itakidhi bei inayotakiwa na Leicester ili wamng’oe.