Haaland rekodi nyingine tamu

MANCHESTER, ENGLAND. STRAIKA wa Manchester City amevunja rekodi nyingine baada ya kufunga hat-trick kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Burnley.

Haaland alifunga mabao 42 na kufunga hat-rick yake ya sita msimu huu wikiendi iliyopita Man City ikiibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Burnley.

Sasa Haaland amefikia idadi ya mabao na hat-trick alizofunga Ronaldo wakati anakipiga Manchester United mwaka ambao alibeba tuzo yake ya kwanza ya Ballon d'Or.

Vile vile Haaland anakaribia rekodi ya Mohamed Salah na Ruud van Nistelrooy katika historia ya Ligi Kuu England, wakali hao wa mabao waliwahi kufunga mabao 44 katika mashindano yote kila mmoja.

Aidha Haaland ana mtihani mwingine wa kufikia rekodi iliyowekwa na nyota wa zamani wa Tottenham, Clive Allen aliyecheka na nyavu mara 49 kuanzia msimu 1986 -1987. Haaland anaifukuzia rekodi nyingine ya Dixie Dean aliyefunga mabao 60 mwaka 1920.

Baada ya rekodi ya Haaland, Pep Guardiola akasema Haalanda atakua tishio zaidi siku za usoni kwasababu mashabiki watatarajia mambo makubwa kutoka kwake.

"Haaland ametisha sana, atakua hatari sana baadaye, lakini nachofahamu Haaland hajali kuhusu maneno ya watu, atafunga mabao mengi, sijui atafunga idadi ya mabao mangapi, mchango wake ni mkubwa, lakini katika maisha yake yake ni kufikiria mambo mazuri, hii inamsaidia sana," alisema Haaland.

Guardiola alimtoa nje Haaland kwenye waliocheza dhidi ya Leipzig wiki iliyopita na kumnyima nafasi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao sita kwenye mechi ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kufunga mabao matano.

Kocha wa Man City, alikosolewa katika hafla hiyo kwa kumnyima mchezaji wake nafasi ya kuvunja rekodi ya Lionel Messi aliyowahi kuweka wakati anakipiga Barcelona. Messi alifunga mabao sita peke yake kati mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen.