Carragher asema Solskjaer afukuzwe tu

Monday October 25 2021
sosha pic

MANCHESTER, ENGLAND. BAADA ya kupokea kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool, staa wa zamani wa Liverpool na mchambuzi maarufu nchini England, Jamie Carragher amesema Manchester United inahitaji kocha mpya ili ishinde mataji.
United ilikuwa na siku mbaya jana, Jumapili baada ya kupokea kichapo cha mabao matano huku  Mohamed Salah akifunga hat-trick.
"Siku chache zilizopita sikuwa na lengo la kumsema vibaya  Ole Gunnar Solskjaer, lakini ni ukweli kwamba hadi kufikia sasa amefanya kazi nzuri sana, lakini ili timu ifike ngazi ya Liverpool, Manchester City na Chelsea inahitaji kupata kocha bora zaidi yake.
"Solskjaer hafai kuwa kocha wa Man United ikiwa wanahitaji kwenda ngazi nyingine kwa sababu sioni ni jinsi gani anaweza kufikia uwezo wa makocha kama Jurgen Klopp, Pep Guardiola na Thomas Tuchel.

Advertisement