Bosi mpya mjini, Haaland anga za wenye pochi nene Ligi Kuu England

Arsenal bana...Wachekelea Haaland kuvaa jezi yao

LONDON, ENNGLAND. MANCHESTER City imenasa saini ya Erling Haaland kwa kitita cha Pauni 51 milioni baada ya kumfukuzia kwa muda mrefu na anatarajia kujiunga nao mwisho wa msimu huu.

Haaland anaondoka Borussia Dortmund akiwa ameifungia jumla ya mabao 85 katika mechi 88 alizocheza tangu alipojiunga nao mwaka 2020.

Licha ya kuonyesha kiwano bora tangu alipokuwa akikipiga RB Salzburg, mkali huyo amezidiwa thamani ya usajili na baadhi ya mastaa ambao hata hivyo wameshindwa kung’ara katika timu zao tofauti na Haaland.

Vilaza hawa wamesajiliwa kwa mkwanja mrefu kuliko Haaland.


Kepa Arrizabalaga —Pauni 71- Chelsea

Licha ya kusajiliwa kwa mkwanja mrefu kipa huyu hakuonyesha cheche msimu wake wa kwanza tu anakipiga Chelsea akitokea Athletic Bilbao na kuachwa kikosi cha kwanza na Frank Lampard wakati anainoa timu hiyo.


Nicolas Pepe — Pauni 72 - Arsenal

Pepe alikuwa na kiwango bora wakati anakipiga Lille, amecheka na nyavu mara 22 Ligue 1 kabla ya Arsenal kumnasa kwa kitita cha Pauni 72 milioni.Hata hivyo kiwango chake kikaporoka tanu alipotua Arsenal licha ya kusajiliwa kwa pesa ndefu badala yake anasugua benchi chini ya Kocha Mikel Arteta.


Romelu Lukaku — Pauni 75m - Manchester United

Wakati Lukaku anajiunga na Manchester united wengi walidhani straika huyo angekuwa moto wa kuotea mbali.kutokana na majeruhi ya kwa mara Lukaku aliachwa kikosi cha kwanza baada ya Jose Mourinho kufukuzanafasi yake ikichukuliwana Ole Gunnar Solskjaer


Eden Hazard — Pauni 88 - Real Madrid

Mashabiki wa Chelsea waliumia Hazard alipojiunga na Real Madrid, wengi waliuponda huo. Winga huyo tangu alipotua Los Blancos hakuonyesha cheche na kundamwa na majeraha huku akisugua benchi.


Antoine Griezmann — Pauni 107- Barcelona

Huu ni kati ya usajili mbovu kuwahi kutokea licha ya kusajili kwa mkwanja mrefu Griezmann hakutuboa kikosi cha kwanza Barcelona.

Tangu alipocheza Camp Nou amefunga mabao 35 katika mechi 120 alizocheza. Kwasasa anakipiga Atletico Madrid kwa mkopo wa miaka miwili.