Arteta aitibulia Japan kisa beki

LONDON, ENGLAND. BEKI wa Arsenal, Takehiro Tomiyasu, ameachwa kwenye kikosi cha Japan kutokana na majukumu ya klabu kwani ametakiwa kurudi England haraka iwezekanavyo.

Tomiyasu alionyesha kiwango kizuri Japan ilipocheza dhidi ya Marekani wiki iliyopita wakatitaifa hilo likipata ushindi wa mabao 2-0 lakini sasa anatahitajika jijini London na kocha wake Mikel Arteta.

Beki huyo anatarajia kurudi London kabla ya mechi ya kirafiki Japan itakapomenyana na Ecuador kesho. Kwa mujibu wa ripoti Tomiyasu hakupata majeraha yoyote bali anatakiwa na kocha kwaajili ya majukumu ya klabu.

Awali mashabiki walipata hofu huenda beki huyo amepata majeraha kwani wana mechi ngumu ya Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham wikiendi hii. Lakini kurejea kwake hakuhusiani na majeraha yoyote.

Hata hivyo Tomiyasu hakuanzishwa katika mechi hata moja ya Ligi Kuu England msimu huu baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua mwishoni wa msimu wa 2021-2022.

Wakati huohuo, kiungo wa Arsenal, Thomas Partey ameumia kwenye mchezo wa kirafiki Ghana ilipocheza dhidi ya Brazil wiki iliyopita. Sasa kiungo huyo ataukosa mchezo huo wa derby wikiendi hii.