Rashford azua hofu Man United

Rashford azua hofu Man United

Manchester, England. Marcus Rshaford anaweza kukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu England wa Manchester United dhidi ya West Ham kutokana na kuumia bega juzi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alilazimika kutoka uwanjani kipindi cha pili katika mchezo wa kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Paris Saint-Germain, akimuacha Ole Gunnar Solskjaer akihangaikia afya yake.

Rashford, ambaye alisawazisha bao la kwanza dhidi ya PSG juzi, alitoa ishara katika benchi kuwa hawezi kuendelea na nafasi yake kuchukuliwa na Paul Pogba.

Solskjaer alisema baada ya mchezo huo: “Ameumia kiasi fulani katika bega lake. Bila shaka anaweza kuwepo katika mchezo ujao dhidi ya West Ham, lakini hatuna uhakika.”

Kutokuwepo kwa mshambuliaji huyo kunaweza kumpa wakati mgumu kucha wa timu hiyo katika upangaji wa safu yake ya ushambuliaji.

Edinson Cavani anakumbana na adhabu ya mechi tatu nje kutokana na maneno yake mtandaoni, licha ya Chama cha Soka England (FA) hakijatoa uamuzi.

Bega la Rashford limekuwa kama tatizo linaloendelea msimu huu, kwani alishawahi kuumia katika vipindi tofauti.

Awali alilazimika pia kukosa michezo ya timu ya taifa ya England kwa kuumia bega alipokuwa akiitumikia Man United dhidi ya Everton.