Liverpool ubingwa ndio basi tena EPL

Monday May 09 2022
Liver PIC

LONDON, ENGLAND. PETER Crouch anaamini ndoto za Liverpool za kubeba ubingwa msimu huu zimeyeyuka baada ya sare ya bao 1-1 iliyopata dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita.

Croach aliyewahi kukipiga Liverpool ameweka wazi kuwa mabingwa watetezi Manchester City wapo katika nafasi nzuri ya kubeba kwa mara nyingine baada ya sare hiyo.

alipoulizwa Crouch kuhusu Liverpool kama itaweza kubeba ubingwa wa msimu huu, straika huyo wa zamani amekiri majogoo wa Anfield wamezingua na amewaodoa kwenye wenye mbio hizo.

“Huo ndio ukweli Lverpool haiwezi kubeba, Man City ina nafasi kwa asilimia kubwa, haipotez mechi kirahisi wala kutoa sare, kabla ya mechi nilisema haitakuwa rahisi mechi rahisi, Tottenham ina wachezaji watatu hatari na wana uwezo wa kufunga wakati wowote,” alisema Croach.

Endapo Manchester City itapata ushindi dhidi ya Newcastle itaiacha Liverpool kwa toafuti ya pointi 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku zikiwa zimebaki mechi tatu kwa upande wao.

Aidha licha ya matumaini yao ya ubingwa kwenye ligi kuyeyuka Liverpool bado ina nafasi ya kumaliza msimu na makombe matatu baada ya kubeba Carabao lakini sasa inaitolea macho ndoo ya FA ambayo itakipiga na Chelsea huku Ligi Mabingwa Ulaya itacheza dhidi ya Real Madrid jijini Paris, Ufaransa katika fainali ya waka huu.

Advertisement
Advertisement