Carragher amvuta Pochettono Old Trafford

Friday November 26 2021
Carra PIC

LONDON, ENGLAND. MKONGWE wa Liverpool, Jamie Carragher ametoa kama ushauri kwa Mauricio Pocettino kuchukuwa mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer aliyefukuzwa kazi wiki iliyopita.

Carragher alisema hayo baada ya kikosi cha Pochettino kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia jana.

Mkongwe huyo amesisitiza utakuwa uhamisho muhimu kwake kwenda kuinoa Man United badala ya PSG.

“Kama atapata nafasi asiichezee, nafasi kama hizi zinakuja mara moja katika maisha yetu, ningekuwa mimi ningekubali, nashindwa kuelewa kwanini anasuasua kufanya uamuzi,” alisema Carragher.

Wakati huo huo, Thiery Henry aliungana na Carragher kuizodoa PSG pamoja na mastaa wake Kylian Mbappe, Neymar Jr na Lionel Messi ambao walishindwa kuonyesha kiwango bora dhidi ya Man City.

“Kama unataka kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huwezi kulinda goli ukiwa na wachezaji saba uwanjani, haiwezekani hata kidogo, kwa mtindo huu PSG haitaweza kubeba kombe lolote,” alisema Henry.

Advertisement

Pochettino anatajwa kama mrithi sahihi wa Solskjaer United.

Advertisement