VAS PINTO AZISHANGAA KBC, TUSKER FC

ZUNGU wa Gor Mahia, Carlos Vaz Pinto kabaki kuzishangaa KCB na Tusker FC timu za pekee ambazo zimekuwa zikibadilishana usukani wa ligi kuu tangu msimu wa 2020-21 ulipoanza.


Wakati KCB na Tusker wakianza kwa vishindo, Gor walikuwa wakihangaika na wakati mmoja mwanya kati yao na vinara wa ligi ilikuwa ni alama 16.


Lakini baada ya kupunguza pengo hilo hadi alama tano ndani ya muda wa wiki mbili, baada ya zile mechi za wikendi iliyopita, Vaz kashindwa kuzielewa KCB na Tusker.


"Wiki chache tu, waliokuwepo kileleni walikuwa wametuacha kwa alama 16 lakini kufikia Jumapili baada ya kuwalima Sofapaka, pengo lilipungua na kusalia na alama tano. Alama 16 ni nyingi sana kuzipunguza hadi tano. Sijui wenzetu wanakwama wapi ila ninachojua, ni kuwa  sisi tumeshika nare na fursa tunayo ya kutetea ubingwa wetu msimu huu," Pinto kachocha.


Katika kipindi hicho cha wiki mbili, Gor wamesajili ushindi wa mechi sita mfululizo na tisa kwa ujumla ukijumulisha na zile mechi za Betway Shield Cup walikofanikiwa kuingia fainalini.
Mwendo wa Gor umempanikisha straika wa zamani wa Tusker FC  ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC ya Tanzania.


"Jamani Gor Mahia wakibeba ubingwa tena msimu huu, yaani bora KCB na Tusker wasambaratishe hizo klabu. Utakuwa mchezo sasa," Ambani kacharuka.