NYOTA WA BORUSSIA DORTMUND AJENGA SHULE MOMBASA

Tuesday May 11 2021
mombasa pic
By Thomas Matiko

WING’A chipukizi wa Borussia Dortmund anayeripotiwa kuwindwa na Manchester United, Jude Bellingham, kakamilisha ujenzi wa shule kule Mombasa.
Kinda huyo mwenye miaka 17, kakamilisha ujenzi wa shule hiyo ya Miche Bora Nursery & Primary School na sasa kaanzisha mchakato wa kuchangisha fedha za kuhakikisha wanafunzi chuoni humo hawakosi msosi.
“Ile shule tuliyokuwa tukijenga Mombasa imekamilika sasasa wanafunzi wanafurahia masomo yao. Nawashukuru wote waliotupa sapoti pamoja na kutoa michango. Mimi pamoja na timu yangu tunashukuru sana.” Bellingham alisema kwenye taarifa aliyoitoa.
Wing’a huyo anayeweza kutumika kama kiungo amekuwa akishirikiana na Mustard Seed Project kwenye kufanikisha mradi huo.
Mumiliki wa Mustard Seed, Rita Flowler anasema Jude alijiongeza kwenye mradi huo baada ya babake mzazi kumdokezea.
“Babake Jude, Mark anafanya kazi nab inti yangu na ndiye aliyemjuza kuhusu mradi huo wa hisani tuliokuwa nao. Babake alipomdokezea Juse hakusita kujiongeza. Ni dogo mngwana sana licha ya umri wake mdogo na ana mapenzi makubwa ya kuwasaidia wasiojiweza.” Fowler aliliambia jarida la The Sun.
Jude anasema sasa mpango wake ujao ni kuhakikisha anasaka fedha zaidi kutoka kwa wahisani wenzake ili kuweza kuwanunua vyakula wanafunzi wa shule hiyo.
Kinda huyo kwa sasa anasemekana kuwinda na Man U, wanaomtaka badala ya Jadon Sancho ambaye wamekuwa wakimfukuzia kwa muda. Hata hivyo baada ya kuona hawatafika bei, wameaumua kumgeukia kinda huyo alieyonyesha dalili za kuja kuwa staa mnoma siku za mbeleni.
Bellingham alijiunga na Dortmund Julai 2020 kwa dau la pauni 20 milioni akitokea Birmingham inayoshiriki divisheni ya pili kule Uingereza.
Tayari amehusika kwenye mechi kadhaa msimu huu kwenye first team ya Borussia ikiwemo Champions League na ndiko walikonea uwezo wake maskauti wa Man U.

Advertisement