KISA DATA BANDO, NYOTA KOGALO WAMGOMEA PINTO

Tuesday April 27 2021
ogalo pic
By Thomas Matiko

GOR MAHIA kumeshindikana na sasa wachezaji wamegomea ukufunzi wa kocha Carlos Vaz Pinto kisa data bando.
Mpaka sasa wachezaji wa Gor hawajalipwa mishahara yao ya miezi mitatu iliyopita na uongozi wa klabu umekiri wazi wazi kwamba hawana fedha.
Baada ya lockdown kuingia, kocha Vaz Pinto kupitia kundi lao la Whatsapp amekuwa akitoa maelekezo ya ukufunzi kwa wachezaji wake ambao wanatakiwa kufanya mazoezi ya kibinafasi kisha kumtumia vikilipu ili aweze kujua wanaendelea vipi.
Lakini sasa idadi kubwa ya wachezaji wa Gor imegomea mpango huo wakidai kwamba hawana fedha za kununua data bando sababu hawana pesa.
“Siku hizi kundi ya WhatsApp ya klabu ipo kimya kweli. Hakuna anayezungumza wala kutuarifu  chochote hadi meneja wa timu. Wachezaji sasa tumelazimika kusaka mbinu zinginezo za kusaka riziki. Hata hayo masuala ya kumtumia kocha video za kipekee za mazoezi ya kibinfasi tumeacha. Utamtumiaje video wakati hata kununua data bando sasa hivi imekuwa noma. Ni pesa za kujikimu utahangaika kusaka au ni za kununua data bando ili umtumie kocha video wakati klabu hata haikulipi.” Kalalama mmoja wa wachezaji anayepania kuondoka mwishoni mwa msimu.
Wachezaji wengi nwa Gor tayari wameweka wazi nia yao ya kujitoa Gor mwishoni mwa msimu huu ili kuikimbia msoto.
Katibu mkuu wa Gor Dolphina Odhiambo kadhibitisha kwamba ni kweli wachezaji wa Gor hawajalipwa mishahara yao. Odhiambo anasema hii ni kwa sababu mdhamini wao Betsafe kazuia kutoa hela toka ligi ilipositishwa.
Hata hivyo safu hii inafahamu kuwa Gor wamebakizia mgao wa Sh4 milioni pekee mwaka huu kutoka kwa Betsafe. Ni fedha ambayo inatosha kugharamia mishahara ya wachezaji wa Gor kwa mwezi mmoja tu.
Odhiambo aidha kawachana mashabiki wa Gor akiwashtumua kwa kupenda kupayuka na kukashifu uongozi wakati wameamua kutoisadia timu na michango au kununua jezi za klabu.


Advertisement