CORONA YAITIBULIA TUSKER FC

Monday March 29 2021
TUSKER PIC
By Thomas Matiko

KUFUATIA kusimamishwa tena kwa ligi kuu ya FKF-PL na Rais Uhuru Kenyatta, ni kipi kinachoweza kutokea?
Rais Uhuru wiki iliyopita alipiga marufuku michezo yote nchini ikiwa mojawepo ya kanuni zilizowekwa kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.
Shirikisho la soka nchini FKF likawa halina budi ila kutia amri na kusimamisha ligi zote nchini hadi pale marufuku hiyo itakapoondolewa.
Na huku zikiwa zimepigwa mechi 16 na pekee, hii ina maana gani kuhusu hatma ya ligi kuu msimu huu wa 2020/21?
Kwenye msimu uliopita 2019/20 Rais Uhuru aliposimamisha ligi kwa zaidi ya miezi sita kufuatia mkuripuko wa virusi hivyo, Rais wa FKF Nick Mwendwa aliishia kuwatawaza Gor Mahia baingwa huku zikiwa zimesalia mechi tu msimu huo ufikie kikomo.
Kulingana na Mwendwa, alichukua uamuzi huo kwa mujibu wa katiba ya FKF ambayo inaeleza kuwa ikiwa msimu umepitisha nusu za mechi zake, na ukasitishwa kwa sababu zozote zile, basi timu iliyopo keleleni ndio watakaotawaza mabingwa.
Msimu huu, zimechezwa mechi 16 mpaka sasa tangazo la Rais Uhuru lilipotoka zikiwa zimesalia mechi tatu mzunguko wa kwanza wa ligi ya msimu huu utamatike.
Ikiwa marufuku ya Rais itadumu kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa msimu uliopita na kutishia kuvuruga msimu ujao wa 2021/21 na hivyo kulazimisha msimu huu ufutiliwe mbali, basi Mwendwa atalazimika tena kuchezesha kifimbo chake kwa mujibu wa katiba ya FKF.
Safari hii, hakutakuwepo na bingwa na itakuwa ni pigo kubwa kwa Tusker FC ambao wamegandia kileleni mwa ligi kwa zaidi ya wiki saba sasa.
“Ikiwa msimu utalazimika kufutiliwa mbali kwa sababu zote zile na itokee kwamba timu zote hazijakamilisha ratiba za mechi zao za mzunguko wa kwanza, basi ligi ya msimu huo itafutwa kabisa.  Lakini ikiwa klabu zote kwenye ligi zitakuwa zimekamilisha ratiba za mechi zao kwenye mzunguko wa kwanza licha ya asilimia 75% ya mechi zote za ligi kuwa zimechezwa, basi msimamo wa jedwali kama ulivyo baada ya mzunguko wa kwanza ndio utakaotambulika rasmi kama matokeo a mwisho ya msimu huo.” Katiba ya FKF inaeleza.
Kando na kusalia na mechi tatu mzunguko wa kwanza wa msimu huu kukamilika, timu kadhaa zilikuwa zimecheza mechi mechi chini ya 16.


Advertisement