Zuchu kama Harmonize kwa Mkapa

MWANADADA anayetanya vizuri kwenye lebo ya (WCB) Zuhura Hassan ‘Zuchu’ amewatanguliza wacheza show wake kwa live band huku yeye akishuka kwa kamba kutoka juu.

Kitendo alichokifanya mwanadada huyo kimeibua shangwe kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo kwa Mkapa.

Zuchu ameshuka kwa kamba akiwa na bendera ya Simba mkononi huku akiwauliza mashabiki wa timu hiyo kuwa je? Wapinzani wataweza.

Kitendo hicho kiliwahi kufanywa pia na msanii nyota Harmonize wakati wa tamasha la Wiki ya Mwananchi mwaka 2020.