Zoran: Kazi iliyobaki tutaimalizia hapa Dar

Thursday August 04 2022
kazi pic
By Eliya Solomon

LICHA ya kukiri kuwa maandalizi ya kikosi chake yalienda vizuri huko Misri, kocha wa Simba, Zoran Manojlovic anaamini kuwa bado  anakazi ya kufanya kwa siku chache zilizosalia.

Zoran ambaye kwenye mazoezi ya  kesho, Ijumaa atakutana na wachezaji wake wote, ikiwemo wale ambao walikuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars alisema amevutiwa na uwajibikaji wa wachezaji wake.

"Mandalizi yapo pazuri, ninafuraha na uwajibikaji wa wachezaji yapo matumaini makubwa tusubiri na kuona msimu utakapoanza,"

 "Ninahamu ya kujumuika na wachezaji wote kumalizia sehemu iliyobaki ya maandalizi," alisema.

Advertisement