Yanga yaunda kamati mpya

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Msimu uliomalizika, Yanga ndio timu iliyoongoza kwa kuingiza idadi kubwa ya amshabiki katika mechi zake za nyumbani ambapo iliingiza jumla ya mashabiki 141,681

Kamati ya utendaji ya Yanga chini ya mwenyekiti wa klabu hiyo Dk Mshindo Msolla imeteua kamati mpya ya matawi, wanachama, hamasa na habari ambayo itaundwa na wajumbe 17 ambao ni wanachama na wapenzi wa timu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Yanga leo, imesema kuwa kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Saad Khimji ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

Mbali na Khimji ambaye pia ni naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Suma Mwaitenda, Dk Athuman Kihamia, Samuel Korosso, Said Side na Victor Vedasto.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Seleman Kigwangala, Deborah Mkemwa, John Sanga, Clifford Lugola, Ramadhan Bendera, Munir Seleman na Bakari Bundala.

Pia kuna Shaban Mgonja, Said Mrisho, Dakota De Lavida na Eliud Mvella.

Kuundwa kwa kamati hiyo ni maboresho ya kamati ya hamasa ya awali ya yanga iliyoundwa Septemba 2019 ambayo ilijumuisha wasanii kadhaa na baadhi ya watu maarufu