Yanga yatoa hali ya hatari

Sunday February 28 2021
yanga princes
By Mustafa Mtupa

ZIKIWA zimebaki siku chache kuelekea mtanange wa Kariakoo Derby kati ya Simba Queens na Yanga Princess, kocha wa Yanga, Edna Lema 'Mourinho' amewapa onyo wapinzani wake.

Akizungumza na Mwanaspoti Online, Edna amesema jambo pekee wanalotakiwa kufanya Simba ni kuhakikisha wanashinda mechi hiyo la sivyo hawatakaa kwa utulivu.

"Ni mechi nzuri lakini siwezi kukwambia chochote, kitu ninachoweza kusema ni kwa kocha wao Mussa Hassan Mgosi kwamba ahakikishe yeye na vijana wake wanashinda mechi hiyo la sivyo siku ya siku ndio watanijua vizuri," amesema na kuongeza,

ssimba qeeen

"Baada ya mechi nitazungumza zaidi, sio sasa na hata kama kutakua na mkutano kabla ya mechi siwezi kuongea sana, zaidi wasubiri tu kitakachotokea uwanjani."

Mchezo huo utakaopigwa Machi 5 kwenye Uwanja wa Karume unatarajiwa kuwa wa kisasi, baada ya Yanga kupoteza mechi nne kati ya tano zilizopita kwa vipigo vya aibu.

Advertisement

Msimu wa 2018/19 mchezo wa kwanza ilifungwa bao 7-0, wa pili ikafungwa  5-1 na uliopita mzungumko wa kwanza ilikula 3-1 na marudiano ikachukua 5-1, lakini msimu huu ilitoka suluhu ya 0-0 kwenye mzunguko wa kwanza.

Advertisement