Yanga waibipu TFF Derby

UONGOZI wa Yanga umesema umepokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuhusiana na kusogezwa kwa mechi kutoka saa 11:00  hadi 1:00 jioni.
Mabadiliko hayo ni kinyume cha kanuni ya 15(10) za Ligi Kuu
 inayohusu taratibu za michezo ambayo unasema mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza Yatajulishwa  ipaaavyo kwa pande zote mbili husika za mchezo angalau masaa 24 kabla ya muda wa awali.
Kutokana hilo uongozi wa Yanga umesema watapeleka timu muda wa awali saa 11:00 jioni,hivyo uongozi wa Yanga umeitakia bodi ya Ligi na TFF kuendesha ligi kwa kuheshimu na kufuata kanuni zinazowekwa.
Basi la timu la Yanga limefika uwanjani saa 10:18, wakati Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mshindo Msolla amefika saa 10:05.