Yanga vs Simba: Mapema tu kibanda umiza kimejaa

Mashabiki wajazana kibanda umiza asubuhi

IKIWA ni saa tano asubuhi na yamebakia masaa mengi kabla ya kufika saa 11:00 jioni ambapo mchezo wa Simba na Yanga utaanza,  tayari mashabiki wamesha jazana kibanda umiza.

Mwanaspoti ilibahatika kufika maeneo ya Tandale kwa Mtogole ambapo moja ya kibanda umiza kimeshajaza tayari.

Mashabiki hao wamekaa kibandani  kuangalia mechi ya marudiano baina ya timu hizo mbili.

Mbali ya mashabiki wanaoangalia marudio ya mechi, wengine  wameweka vikundi vya mabishano.

Mmoja kati ya mashabiki hao alikuwa akitamba banda zima na kuonyesha staili ya ushangiliaji ya mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele.

Shabiki mwingine  amesema leo ndio siku ambayo nyama ya Simba itapikwa na kuliwa kama nyama ya mbuzi.