Yanga, Namungo ngoma ngumu

Muktasari:

Mambo yamekuwa magumu kwa Namungo na Yanga baada ya timu hizo kwenda mapumziko zikishindwa kufungana.

Mambo yamekuwa magumu kwa Namungo na Yanga baada ya timu hizo kwenda mapumziko zikishindwa kufungana.
Mechi baina ya timu hizo Imekuwa ngumu Kila zinapokutana na hata Leo hali imekuwa hivyo hivyo.
Timu zote zilianza mchezo  kwa kasi na dakika ya Tano tu Yanga ilifika golini kwa Namungo lakini passi Safi ya Said Ntibazonkiza 'Saido' ilishindwa kumaliziwa na Michael Sarpong.
Namungo ilijibu mashambulizi dakika ya 8 lakini Hashim Manyanya alishindwa kufunga akiwa katika nafasi nzuri na baada ya kupiga pasi iliyotoka nje kidogo ya lango.


Yanga ilionekana kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Namungo  kipindi Cha kwanza lakini washambuliaji wake walioongozwa na Yacouba Sogne na Michael Sarpong walishindwa kuwa na akili ya kumalizia vizuri
Timu hiyo ilikuwa ikitengeneza mashambulizi kupitia kwa Saido na Tuisila Kisinda lakini Kila walipofika golini washambuliaji wa Yanga walishindwa kufanya uamuzi nzuri wa kutumbukiza Mpira wavuni.


Dakika ya 17 Said alipiha Kona ambayo iliokolewa na mabeki wa Namungo huku mrundi huyo akishindwa kufunga dakika ya 22 akiwa katika nafasi nzuri  baada ya kupata pasi ya Tuisila.
Katika kipindi Cha kwanza Yanga imepata Kona sita dhidi ya moja ya Namungo lakini imeshindwa kuzitumia vizuri baada ya mabeki wa Namungo kuwa imara kuokoa hatari zote.
Mabeki wa Namungo walioongozwa na  Stephen Duah,Frank Maging,Fred Tangalo na Jafar Mohamed walicheza vizuri katika kipindi Cha kwanza na kuwa kikwazo kwa Safi ya ushambuliaji ya Yanga.


Hata hivyo timu hiyo ilionekana kupata shida kwenye safu Yao ya ushambuliaji kwani ilikosa ubunifu na kujikuta ikipiga shuto moja tu golini kwa Yanga tena lisilolenga lango.
Kitendo Cha Namungo akishindwa kufika mara kwa mara golini kwa Yanga kulisababisha safu ya ulinzi ya Yanga chini ya Bakari Mwamnyeto na Dickson Job kutokuwa na presha.