Yanga: Hatukuwa na maandalizi mazuri

Sunday September 12 2021
feli pic

PICHA NA LOVENESS BERNARD

By Imani Makongoro

Uongozi wa Yanga umekiri timu yao haikuwa na maandalizi mazuri ya msimu mpya.

Uongozi umebainisha hayo baada ya Yanga kuruhusu kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wanajipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano Septemba 19 nchini Nigeria.

"Leo tumepoteza mechi ya nyumbani, tunakiri maandalizi yetu ya pre season hayakuwa mazuri, ni kama hayakuepo ila tunajipanga," amesema.

Kocha Nabi aliwahi kubainisha kuwa hajapata muda wa kutosha kwenye maandalizi ya timu yake iliporejea nchini ikitokea Morocco ilipoweka kambi ya muda mfupi ikiwa ni siku kadhaa kabla ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Zanaco ambayo pia Yanga ilipoteza kwenye uwanja wa Mkapa.


Advertisement
Advertisement