Winga Azam atambia ushindani

Huyo Tepsi ndo kwanza kaanzaa

KWA namna ulivyo ushindani wa namba kwenye kikosi cha Azam FC, winga wa timu hiyo, Tepsi Evance anauchukulia kama moja ya kukomaza kiwango chake na kutojisahau kujituma ili aendelee kupata nafasi ya kucheza.

Akizungumza na Mwanaspoti, mchezaji huyo alisema anajifunza mengi kwa wachezaji wa ndani na nje, na hujikuta anapata nguvu ya kupigania ndoto zake za kucheza kwa kiwango cha juu ndani na nje.

“Penye ushindani lazima kiwango kinakuwa juu. Ndio maana kila ninapopata nafasi ya kucheza, nazingatia nini kocha anataka kwangu ili aendelee kuniamini kwamba naweza nikaifanya kazi vizuri,” alisema.

“Najifunza mengi kutoka kwa wakubwa zangu walionitangulia. Pia natamani kila ninapocheza nakuwa na vitu vipya na ubunifu utakaonisaidia kutimiza ndoto ya kuwa mchezaji mkubwa.”

Pamoja na ushindani, alisema mazoezi kwake ni sehemu ya maisha na anaaamini yana nafasi kubwa ya kumfanya awe fiti kwa ajili ya kutimiza majukumu.

“Lazima kujitoa kwenye mazoezi, nje na hapo inakuwa kazi ngumu pia kujua kitu gani kocha anapokuwa nafasi anakihitaji umnfanyie, hayo mambo kwangu nayazingatia zaidi,” alisema.