Wachoraji waitwa sherehe za Fifa Qatar

Tuesday September 28 2021
QATAR PIC
By Nasra Abdallah

Wasanii fani ya uchoraji nchini Tanzania wamepata mualiko wa kuhudhuria sherehe za  maandalizi ya kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwaka 2222.
Wasanii hao watakaokidhi vigezo hususani wanaopotambuliwa na Baraza watalipiwa gharama za usafiri pamoja na malazi na kituo hiko.
Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko, katika taarifa yake, aliyoitoa leo Jumanne Septemba, 2021 kwa umma ambapo alieleza kuwa kuna nafasi za watu saba.
Mniko amesema mwaliko huo umetoka kituo cha utamaduni cha Qatar na kutaja wasanii wanaotakiwa ni wa fani za uchoraji wa picha, uchoraji wa Curiculture, uchoraji wa Graffiti, uchoraji wa picha za 3D na Pantomine.
“Kufuatia fursa hii, Basata inawaalika wasanii wa fani  tajwa hapo juu kujitokeza na kuwasilisha nyaraka za kazi zao kupitia barua pepe ya Basata kabla ya kesho Septemba 28, 2021 saa sita mchana.

Advertisement