Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu waitega Yanga

MZIZE Pict

Muktasari:

Taarifa kutoka Misri, zinaeleza sababu ya mabosi wa Zamalek kulipa kiasi hicho cha fedha kwa mafungu ni kutokana na kuihitaji pia saini ya mshambuliaji wa DR Congo, Ben Malango aliyeachana na Qatar inayoshiriki Ligi ya Qatar Stars.

MABOSI wa Zamalek ya Misri wanataka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja baada ya kuripotiwa kukaribia kuipata saini ya nyota wa Yanga, Clement Mzize kiasi kikubwa cha pesa, kitakachomfanya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa kutoka Misri, zinaeleza sababu ya mabosi wa Zamalek kulipa kiasi hicho cha fedha kwa mafungu ni kutokana na kuihitaji pia saini ya mshambuliaji wa DR Congo, Ben Malango aliyeachana na Qatar inayoshiriki Ligi ya Qatar Stars.


Hata hivyo, Zamalek inaelezwa italipa fedha hizo kwa awamu mbili na ya kwanza italipa Dola 375,000 sawa na Sh991 milioni, huku kiasi kitachobakia kitalipwa kuanzia Januari 2026, ili kuipata saini ya nyota huyo hatari kwa sasa nchini.

Qatar ilithibitisha kuachana rasmi na Malango sawa na Percy Tau ambao kwa sasa ni wachezaji huru, hivyo Zamalek inaangalia uwezekano wa kumpata nyota huyo sambamba na Mzize ili wakatengeneze pia safu kali ya ushambuliaji msimu ujao.

Mabosi wa Zamalek wanaamini wana uwezo wa kumpata Malango aliyewahi kutamba na timu mbalimbali zikiwemo, TP Mazembe na CS Don Bosco zote za kwao DR Congo, Raja Casablanca ya Morocco kisha baadaye kujiunga na Sharjah ya Falme za Kiarabu.

Miamba hiyo ya Misri sio ya kwanza kujitokeza kuwania saini ya Mzize kwani hivi karibuni, Wydad Casablanca ya Morocco na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini pia zilionyesha nia ya kumhitaji mshambuliaji huyo mwanzoni mwa msimu kabla ya kubakia.

Awali ilidaiwa Kaizer Chiefs inayonolewa na aliyekuwa Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi aliyempandisha na kumpa pia nafasi zaidi, iliweka Dola 200,000 sawa na Sh542.3 milioni, ofa ambayo mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu waliitupilia mbali.

Kwa upande wa Wydad Casablanca ambayo awali ilikuwa ikifundishwa na Kocha, Rhulani Mokwena wa Afrika Kusini nayo iliweka kitita cha Dola 100,000 (Sh271.1 milioni) huku viongozi wa Yanga wakihitaji Dola 1 milioni sawa na zaidi ya Sh2 bilioni.

Katika msimu wake wa kwanza nyota huyo yaani 2022-2023, alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na mbali na hilo, alichangia upatikanaji wa mabao yake sita, akifunga matano na kuasisti moja kati ya 61 ya timu nzima.

Msimu huo, Yanga ilifika hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kukosa ubingwa kwa faida ya bao la ugenini mbele ya USM Alger ya Algeria kufuatia sare ya jumla ya mabao 2-2, ikichapwa nyumbani 2-1, kisha ugenini ikashinda 1-0.

Msimu wake wa pili wa 2023-2024, Mzize alichangia mabao 13, baada ya kufunga sita na kuasisti saba kati ya 71, ya kikosi hicho kizima, kilichotwaa tena ubingwa wa Ligi Kuu Bara ukiwa ni wa tatu mfululizo kufuatia kukusanya pointi zake 80.

Katika misimu mitatu, huu ndio bora zaidi kwa mshambuliaji huyo kwani hadi sasa amechangia mabao 16, ya Ligi Kuu Bara kati ya 71, yaliyofungwa na kikosi hicho kizima kinachoongoza msimamo, baada ya kufunga mabao 13 na kuasisti matatu tu.