VIDEO: Mwili wa baba yake Boxer kuzikwa leo, Yanga wafanya sala

BEKI wa Yanga, Paul Godfrey 'Boxer' ameibua simanzi baada ya kuwasiri katika Hospital ya Temeke kuchukua mwili wa baba yake aliyefariki dunia Ijumaa.

Yanga wafika katika msiba wa baba mzazi wa "Boxer" Hersi atoa neno

Boxer ndiye aliyekuwa anasubiriwa ili kuhakikisha anashuhudia mazishi ya baba yake yanayotarajiwa kufanyika saa 10 jioni kwao Mbagala.

Hakupata muda wa kuzungumza chochote zaidi ya kupokea pole kutoka kwa nyota wenzake ambao pia walikuwa na nyuso za huzuni.

Viongozi na wachezaji kabla ya kubeba jeneza lililobeba mwili wa Godfrey walifanya sala kwa pamoja na kumpa pole mchezaji mwenzao.

Mjumbe wa kamati ya mashindano Yanga, Mhandisi Hersi Said anasema hawakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kumsindikiza beki huyo kuchukua mwili wa baba yake tayari kwaajili ya mazishi.

“Amepata msiba wakati mbaya akiwa kwenye majukumu hivyo hawakuwa na namna nyingine ya kumuacha peke yake ndio maana tumefika wote eneo la tukio ili kumfariji,” anasema