VIDEO: Mashabiki Yanga nyomi Airport, Polisi waimarisha ulinzi

Sunday June 26 2022
mashabiki pic
By Charity James

NYOMI la mashabiki wa Yanga wamegeuka gumzo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambako wamekuja kuwapokea wachezaji wao baada kukabiziwa taji la Ligi Kuu msimu huu.Yanga jana wamekabiziwa taji hilo baada ya kukubali sare ya bao 1-1 kutoka kwa wenyeji Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mashabiki hao wa Yanga wameanza kujazana nje ya uwanja huo kuanzia saa moja huku wakiwa wanapiga vingoma na kuimba nyimbo za uningwa wakisubiri muda wa kuruhusiwa kuingia ndani.FFU WAMWAGWA KUONGEZA USALAMA

Difenda tatu za zikiwa zimebeba Polisi mbili zimeingia ndani moja imebaki nje kutuliza ghasia za mashabiki ambao wamesimama kando kando ya barabara.

Polisi hao wanakazi kubwa ya kufanya kutokana na nyomi ya iliyojitokeza ambayo inasababisha foleni eneo la kituo cha daladala cha magari yanayoenda Gongo la mboto.

Advertisement