Vibaka nao wako kazini msafara wa Yanga

Wakati mashabiki wa Yanga wakiwa katika msafara kundi la vibaka nalo lipo kazini wakipambana na hali yao.

Mmoja wa watu aliyedhaniwa ni kibaka alijikuta katika wakati mgumu baada ya kukimbizwa na mashabiki nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere 3.

#LIVE: Mapokezi ya UBINGWA YANGA muda huu....!!!!!!



Kibaka huyo baada ya kuona hali ya hatari kwa maisha yake alikimbilia kibanda cha askari wa usalama kisha kukaa chini ya askari hao.

"Askari nisaidieni wataniua hawa mimi sijaiba nisaidieni, wataniua hawa," alisikika mtu huyo akiwaomba msaada askari wa usalama.

Hata hivyo mashabiki hao walipunguza jazba na kutulia huku wakiwataka polisi kumpeleka ndani wakidai alitaka kuiba simu.

šŸ”“#LIVE: SHEREHE za UBINGWA YANGA muda huu....!!!!!! KIMEWAKAAAA


Shabiki mwingine aliyekuwa na kisu alishtukiwa na polisi kisha kumkamata na kumpokonya ingawa baadaye walimuachia huku kisu hicho kikibaki mikononi kwa polisi.

"Nilikuwa namenya viazi nimesahau nimeondoka nacho (kisu) nisameheni Yanga imenichanganya hii," alisikika shabiki huyo akijieleza mbele ya polisi.

Askari wa jeshi la polisi wamekuwa makini kwenye kuimarisha usalama katika maelfu ya mashabiki hao ambao wamefurika barabarani kupokea timu ya Yanga baadaya kuchukua taji la Ligi Kuu Bara jana wakitokea jijini Mbeya.