Vaibu mashabiki kwa Mkapa

Saturday August 06 2022
ndani pic
By Olipa Assa

VAIBU la mashabiki wa Yanga limeanza ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, wakisubiri timu yao kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Vipers ya Uganda.

Yanga inahitimisha tamasha la Wiki ya Mwananchi, ambapo mashabiki walianza kufika asubuhi licha ya mechi hiyo kuanza saa 1:00 usiku, haikuwa sababu ya wao kuchelewa.

Vigoma, mavuvu zera na makofi  vimetawala ndani ya dimba la Mkapa kwa mashabiki waliyofanikiwa kuingia.

Tayari imeanza kuchezwa mechi ya kirafiki kati ya Yanga Princess na Ilala Queens.
Wakati huo huo wachezaji wa Yanga B ambao walivalia jezi nyeusi wamezunguka uwanja mzima kusalimia mashabiki wao.

Advertisement