Uwanja wa Ushirika wafungiwa, Polisi kuhamia Karatu

Moshi. Timu ya Polisi Tanzania Fc italazimika kucheza mchezo wake wa Kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara nje ya uwanja wa nyumbani kutokana na changamoto ya uwanja.


Hayo yanajiri wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wake  wa Jumatano dhidi ya KMC Fc ambao umepangwa kuchezewa wilayani  Karatu badala ya uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi baada ya viongozi wa TFF kuukagua uwanja huo ambao huenda mchezo unaofuata kati ya  Polisi Tanzania Fc na Azam FC ukachezewa hapo.


Akizungunza na vyombo vya Habari, Makamu Mwenyekiti wa timu ya Polisi, Robert Munisi ameeleza kutoridhishwa kwa kuhamishwa Kwa mchezo huo kutokana na kuchelewa pia kupewa taarifa za mahali ulipohamishiwa.


"Tutaenda kucheza mchezo wetu dhidi ya KMC wilayani  Karatu licha ya kwamba kuna umbali ikilinganishwa tumechelewa kupewa taarifa na Shirikisho la mpira wa miguu TFF hivyo tumejiandaa vyema katika kushinda mchezo wetu,mashabiki wetu watakaoweza kuungana nasi waje Karatu." alisema Munisi


Kwa upande wake Ofisa habari wa timu hiyo ya Polisi Tanzania Hassan Juma alisema timu imejiandaa vyema na mchezo huo dhidi ya kutokana na mazoezi waliyofanya wachezaji na maelekezo ya mwalimu na kocha wa timu Malale Hamsin


Hussein Laizer ni Meneja wa Uwanja huo wa Ushirika ambapo alisema jitihada mbalimbali zimefanyika ili uwanja huo uweze kutumika katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada yavkuukagua TFF wamesema ndani ya siku chache unaweza ukatumika Kwa mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania bara.


"Uwanja huu umekua ukitumika katika shughuli mbalimbali za chuo na kiserikali hivyo unaendelea kutunzwa vyema ili u
lete tija kwa watumiaji" alisema Laizer