Straika wa Gwambina aingia na bao

Tuesday April 20 2021
gwambina pic
By Thomas Ng'itu

KOCHA Mohamed Badru ameonyesha kustahili tuzo ya kocha bora wa mwezi Machi baada ya kucheza pata potea  katika mchezo wao na Yanga na kufanikiwa.

Kocha huyo alifanya mabadiliko dakika 48 kwa kumtoa Japhet Mayungu na kuingia Jimson Mwanuke mabadiliko ambayo yalizaa bao dakika 49.

Winga huyo aliingia na mpira wakewa kwanza alipokea pasi kwa Paul Nonga na yeye kukimbia mpaka nje ya boksi na kutulia na mpira kisha aliachia shuyi lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Bao hilo lilidumu kwa dakika tatu tu (52),baada ya beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto kusawazisha na kufanya matokeo yakiwa 2-1 huku mpira ukiendelea.

Kikosi cha Gwambina kilikuwa kikiendana na kasi ya Yanga muda wote bila kuonyesha uchovu wowote licha ya kuwa nyuma kwa bao moja.

Advertisement